Psalms 74:3-7


3 aGeuza hatua zako kuelekea magofu haya ya kudumu,
uharibifu wote huu ambao adui ameuleta pale patakatifu.


4 bAdui zako wamenguruma pale ulipokutana nasi,
wanaweka bendera zao kama alama.

5 cWalifanya kama watu wanaotumia mashoka
kukata kichaka cha miti.

6 dWalivunjavunja milango yote iliyonakshiwa
kwa mashoka na vishoka vyao.

7 eWaliteketeza kabisa mahali pako patakatifu,
wakayanajisi makao ya Jina lako.
Copyright information for SwhKC